Jitambulishe (Identify Yourself)

JITAMBULISHE Uovu kweli tumelimbikiza Yaliyomuhimu kuyapuuza Aushi ya wengi kuteketeza Matendo yetu kutochunguza Thamani yake tukaipunguza Bila shaka katamalaki kiza Lakini haya ni' kasababisha? Umeokoka, uovu waelimisha Lisilohalali kuamrisha Wanyonge si haba wadhalilisha We' huoni wastaajabisha? Jalali mbona wamsambaratisha? Habari njema uliipokea Uka'koka pasi kuchechemea Ukweli hukusita kutetea Majaribuni mwovu kakemea Hivi sasa, mbona ukapotea? Au pia, yepi yalitokea? Kanisani wengi 'mechanganya Ukweli wote 'mewanyang'anya Kwa njia moja uliwakusanya Kwa njia Saba umewatawanya Kapuuza na hata walokukanya Ona sasa umejichanganya! Japo kiza kweli katamalaki Kwake Mola sitingiziki Ukweli wake nitaumiliki Neno lake halibadiliki N'taongeza na visisitizi Kwake ng'o sibanduki! Ni kweli dunia yabadilika Huu ni ukweli usopingika Lakini je, mbona watingizika? Yakupasa vyema kueleweka...